Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CAR yatakiwa kuheshimu tarehe ya uchaguzi:UM

CAR yatakiwa kuheshimu tarehe ya uchaguzi:UM

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeitaka Jamhuri ya Afrika ya kati (CAR) kuandaa duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais na ule wa bunge kulingana na tarehe iliyopangwa kufanyika uchaguzi huo.

Uchaguzi huo ambao unatarajiwa kuandaliwa tarehe 23 Jamuari mwakani umekuwa ukihairishwa kila mara. Kupitia kwa ujumbe na rais wake balozi Susan Rice, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limayataka makundi ya kisiasa na ya kijeshi kujiunga kwenye jitihada za kuleta umoja katika taifa hilo.

Ameitaka serikali kuendelea na maandalizi ya kundaa uchaguzi ulio huru na wa haki.Pia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito kwa tume huru ya uchaguzi kundelea na jitihada zake za kuandaa uchuguzi huo kulingana na maelewano ya washika dau wote.