Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amkumbuka mwanadiplomasia Richard Holbrooke

Ban amkumbuka mwanadiplomasia Richard Holbrooke

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea masikitioko yake kufuatia kifo cha mwanadiplomasia wa Marekani Richard Holbrooke.

Ban ametuma risala za rambi rambi kwa familia ya Richard Holbrooke, mwanadiplomasia wa miaka mingi wa Marekani aliyeaga duinia siku ya Jumatatu. Ban amemtaja Holbrooke kama bingwa ambaye alitoa hamasisho kuhusu ugonjwa wa ukimwi wakati akihudumu kama balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa.

Ban amesema kuwa Holbroke alifahamu umuhimu wa Umoja wa Matifa suala ambalo alilitia msukumo kuhakikisha mafanikio yake.