Adha ya uchumi yamepunguza kiwango cha mishahara:ILO

15 Disemba 2010

Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la kazi duniani ILO inasema kiwango cha kuongezwa mishahara duniani kimekatwa kwa nusu mwaka 2008 na 2009.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ‘Global Wage Report 2010/2011 iliyokusanya takwimu kutoka nchi 115 zinazowasilisha asilimia 94 ya watu wanaokadiriwa kufikia bilioni 1.4 wanaolipwa mishahara duniani , matatizo ya mdororo wa uchumi imepunguza kiwango cha mishara kwa mwezi ambapo kwa wastani ni kutoka asilimia 2.8 mwaka 2007 na kushuka hadi asilimia 1.5 mwaka 2008 na asilimia 1.6 kwa mwaka 2009.

Ripoti inasema ukiitoa Uchina kwingineko ongezeko la mishara limepungua kwa asilimia 0.8 2008 na asilimia 0.7 mwaka uliopita. Ripoti hiyo pia imetoa mtazamo kutokana na mabara na kusema wakati maeneo kama Ulaya Mashariki na Asia ya kati kiwango kikiteremka sana kwingineko kama Amerika ya Kusini hali ni ya kuridhisha.

Mkurugenzi mkuu wa ILO Juan Somavia anaesema ripoti hii inaainisha sura nyingine ya matatizo ya ajira. Akitoa mtazamo wa siku za usoni Somavia amesema kuimarika kwa hali hii kuitategemea kiwango jinsi familia zinakavyoweza kutumia mishahara yao katika kuongeza matumizi.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter