Maisha ya watoto Sudan Kusini yako hatarini:UNICEF

Maisha ya watoto Sudan Kusini yako hatarini:UNICEF

Uhai kwa watoto Sudan Kusini umeelezewa kuwa ni moja ya ulio katika kiwango cha chini kabisa duniani, huku kila motto mmoja kati ya saba wanakufa kabla ya kufikisha umri wa miaka mitano, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Njaa, utapia mlo na malaria ni miongoni mwa sababu kubwa zinazokatili maisha ya watoto Sudan Kusini. UNICEF inasema eneo hilo pia linapata fursa ndogio ya chanjo duniani ikiwa ni asilimia 10 tuu ya watoto wote ndio wanaochanjwa kukinga maradhi mbalimbali.

Mkuu wa UNICEF Sudan Kusini ni Yasmin Ali Haque ambaye anasema kuna jaha ya haraka ya kuongeza misadda ya maendeleo kulisaidia jimbo hilo kukabili changamoto zilizopo.

(SAUTI YA YASMIN ALI HAQUE)

UNICEF inasema inaongeza msaada kwa ajili ya watoto, kina mama na wakimbizi wa ndani kwa ajili ya kuwasaidia endapo kutazuka ghasia baada ya kura ya maoni inayotarajiwa Januari 2011.