Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia huenda zikazuka kufuatia kutajwa washukiwa wa machafuko Kenya:OCHA

Ghasia huenda zikazuka kufuatia kutajwa washukiwa wa machafuko Kenya:OCHA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA ofisi ya Kenya limesema kutajwa kwa watu sita wanaoshukiwa kuchagiza machafuko ya baada ya uchaguzi Kenya kunaweza kuzusha ghasia katika baadhi ya jamii.

OCHA inasema na endapo ghasia zitazuka basi zitakuwa na madhara makubwa kwa binadamu, na hivyo jumuiya hiyo ina mipango maalumu iliyo tayari ili kuhakikisha kwamba watakuwa tayari kuwafikia na kuwasaidia watakaohitaji msaada na watakaoathirika endapo kutazuka ghasia. Lakini Wakenya wenyewe wanasemaje kuhusu hatua hii ya ICC?

(SAUTI MAONI YA WAKENYA)