Skip to main content

Muda wa mahakama za kimataifa za uhalifu umeongezwa:UM

Muda wa mahakama za kimataifa za uhalifu umeongezwa:UM

Muda wa majaji wanaohudumu kwenye mahakama za Umoja wa Mataifa za uhalifu dhidi ya vita vya Balkans vya miaka ya 1990 na mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 wameongezewa muda.

Majaji hao ni wale wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa iliyokuwa Yugoslavia zamani ICTY na wa mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za mauaji ya kimbari ya Rwanda ICTR, ambao muda wao ulikuwa unamalizika mwishoni mwa mwaka huu wa 2010.

Tangu kuanzishwa miaka 17 iliyopita mahakama ya ICTY iliyoko The Hague Uholanzi imeshawahukumu watu 161 kwa uhalifu wa vita uliotekelezwa Yugoslavia ya zamani. Mahakama ya ICTR iliyoko Arusha Tanzania inahukumu watu waliohusika na mauaji ya kimbari na ukiukaji mwingine wa haki za binadamu za kimataifa uliotekelezwa Rwanda 1994.