Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muda wa huduma za afya za dharura Pakistan kuongezwa:IOM

Muda wa huduma za afya za dharura Pakistan kuongezwa:IOM

Wataalamu wa afya wanaotoa huduma za matibabu ya dharura nchini Pakistan nchi ambayo ilikubwa na mafuriko yaliyoharibu kabisa mifumo yote ya afya, wataendelea kubaki nchini humo hadi hapo May 2011.

Tayari nchi za Marekani na Canada zimetoa jumla ya dola 850,000 ambazo zitatumiwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili kuratibia shughuli za kuendelea kuwahifadhi wataalamu nchini humo. Mpango huo mpya utakaonza Janury mwakani, unalengo la kutaka kukarabati upya baadhi ya maeneo yaliyoharibiwa na mafuriko hayo pamoja na kujenga vituo vya afya katika majimbo ya Sindh na Punjab.

Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM litasimamia miradi inayoendeshwa kwa ajili ya kuboreshwa vituo vya afya kwa kufunga vifaa vya kisasa na vyenye uwezo mkubwa.