Skip to main content

Mafunzo dhidi ya usafirishaji haramu wa watu yafanywa Guinea Bissau

Mafunzo dhidi ya usafirishaji haramu wa watu yafanywa Guinea Bissau

Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM, limenza kuendesha mafunzo ya siku tatu kwa wataalamu mbalimbali nchini Guinea Bissau watakaotumika kuwasadia watu waliokubwa na matatizo ya usafirishaji haramu wa binadamu.

Mafunzo hayo yanayofanyika katika mji wa Bafata, yanawashirikisha wawakilishi toka vyama vya kirai pamoja na taasisi za kiserikali ambao wanapewa ujuzi namna ya kuwasaidia watoto waliokubwa na biashara hiyo haramu ya usafirishaji.

Mafunzo mengine kama hayo yalifanyika mwezi uliopita katika mji wa Gabu ikiwa ni miongoni mwa maeneo machache nchini humo yenye idadi kubwa ya waathirika wa vitendo vya usafirishaji. Mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa IOM ya kukabiliana na vitendo hivyo vya usafirishaji haramu binadamu duniani kote.