Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wana mchango mkubwa katika jamii:IOM

Wahamiaji wana mchango mkubwa katika jamii:IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linazitaka serikali kutambua umuhimu wa uhamiaji na kutoa ujumbe huo kwa wananchi.

Shirika hilo limeyasema hayo katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya wahamiaji Desemba 18. Limeongeza kuwa mara nyingi manufaa yanayopatikana kutoka kwa wahamiaji hayatambuliwi kwa kuwa nchi hulichukulia swala hili kama mzigo au kuwapoteza wataalamu wao.

Kulingana na utafiti uliofanywa na chuo kimoja nchini uingereza ulionyesha kuwa wahamiaji kutoka mashariki mwa ulaya walilipa asilimia 37 zaidi ya mapato yao kama ushuru kati ya mwaka 2008 na 2009.

Utafiti huo pia ulionyesha kuwa wahamiaji wengi walisadia kuto huduma muhimu kwa umma kama madaktari , wauguzi au watoa usafi katika idara ya afya. Hii ni kati ya tafiti zilinazoonyesha mchango unaotolewa na wahamiaji kwenye uchumi wa Uingereza.