Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hungury yajiandaa kuwa Rais wa EU na UNHCR yatoa mapendekezo

Hungury yajiandaa kuwa Rais wa EU na UNHCR yatoa mapendekezo

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR hii leo linachapisha mapendekezo kwa taifa la Hungary linapojiandaa kuchukua urais wa umoja wa Ulaya Januari mwakani.

Wakati Umoja wa Ulaya unapoendelea na juhudi za kuwa na hifadhi ya pamoja nayo UNHCR inaitaka Hungary kuongoza kwenye jitihada za Umoja wa Ulaya kwa usalama wa kimataifa. Inapochukua urais Hungary pia itaridhi mjadala mkali kuhusu mabadiliko ya kisheria na changamoto zilizopo kuhusiana na kuwepo kwa hifadhi katika Umoja wa Ulaya.

UNHCR kwa sasa inaishauri Hungary kuhakikisha kumeafikiwa makubalino kwenye mabadiliko ya sheria zinazohusiana na hifadhi katika Umoja wa Ulaya kuambatana na sheria za kimataifa.