Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Iraq imetoa msaada kwa waathirika wa mafuriko Pakistan

Iraq imetoa msaada kwa waathirika wa mafuriko Pakistan

Serikali ya Iraq imetoa msaada wa tani 4000 za unga wa ngano kwa shirika la mpango wa chakula duniani WFP ili kuwasaidia waathirika wa mafuriko nchini Pakistan.

Unga huo wa ngano ulio na thamani ya dola milioni 1.6 ni msaada wa kwanza wa Irak kwa WFP wa juhudi za kuchangia katika misaada ya kibinadamu nje ya Iraq.

Nchini Iraq kwenyewe serikali inatoa zaidi ya asilimia 50 ya fedha zote zinazotumika kwa chakula mashuleni na miradi ya misaada kwenye maeneo yaliyoathirika sana na machafuko. Mwaka huu wa 2010 Iraq imechangia dola milioni 17 kuunga mkono mpango wa chakula mashuleni ambao umeshawafikia watoto zaidi ya laki tano.