Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zichukuliwe kutuliza machafuko Darfur:UNAMID

Hatua zichukuliwe kutuliza machafuko Darfur:UNAMID

Vikosi vya kulinda amani vya muungano wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika nchini Sudan UNAMID vimetaka kuimarika kwa hali usalama na kuanzishwa duru ya kutatua kero kufuatia kuzuka kwa mapigano baina ya vikosi vya serikali na vile vya waasi.

Mapigano hayo yaliyoduma kwa muda wa saa 24 yamehusisha kikosi cha Sudanese armed forces na kile cha waasi wa eneo la Darfur ikiwa ni tukio la pili kutokeo kwenye kijiji cha Khor Abeche, kilichopo umbali wa kilimita 800 kutoka Kaskazini mashariki kwa jimbo hilo la Darfur.

Kiongozi wa muungano wa vikosi hivyo vya kimataifa UNAMID Ibrahim Gambari ametaka uongozi kushughulia ghasia hizo kwa kuanzisha duru ya masikizano ili kuepusha hali kama hiyo kujitokeza hapo baadaye.Watu kadhaa walijeruhiwa na baadhi ya nyumba kuchomwa moto kufuatia ghasia hizo.UNAMID imezitaka pande zote kujiepusha na hatua zozote kofori.