Skip to main content

Mshauri wa UM kuhusu michezo ahofia kufungwa kwa NGO ya vijana Gaza

Mshauri wa UM kuhusu michezo ahofia kufungwa kwa NGO ya vijana Gaza

Mshauri maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu michezo kwa maendeleo na amani bwana Wilfried Lamke amelezea hofu yake kuhusu kufungwa kwa nguvu ofisi zote za Sharek Youth Forum ambazo sio za kiserikali zinazohusika na masuala ya vijana.

Shirika hilo lisilo la kiserikali linashirikisha watoto na vijana 60,000 pamoja na wakufunzi wa michezo wa kujitolea 2000 mbali ya michezo pia shirika hilo linatoa msaada wa kielimu. Bwana Lemke ametoa wito wa kuruhusu kuanza tena mara moja kwa shughuli za Sharek Youth Forum bina masharti yoyote kwenye ukanda wa Gaza.