Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lengo la milenia la kutokomeza maradhi bado ni changamoto nchini Tanzania

Lengo la milenia la kutokomeza maradhi bado ni changamoto nchini Tanzania

Ikiwa imesalia miaka 5 tuu kabla ya kufikia 2015 muda wa mwisho uliafikiwa na viongozi wa dunia kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia, kila nchi hivi sasa inajitahidi japo kufikia nusu ya malengo hayo.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa ingawa malengo yote ni muhimu lakini lengo nama 1 ambalo ni kutokomeza umasikini na njaa na lengo namba 6 kutokomeza maradhi yanaonekana kuwa muhimili wa malengo mengine. Lengo namba sita ambalo linagusia ukimwi, kifua kikuu na malaria ndilo lililo na shida kubwa hasa katika nchi zinazoendelea.

Takwimu za karibuni za shirika la afya duniani WHO zimeonyesha kuwa hatua inapigwa lakini bado kuna kibarua. Nchini Tanzania kwa mfano bado inakabiliwa na changamoto kubwa ya kufikia shabaya ya lengo nambari 6. Kila kati ya watu 10 nchini humo mmoja au wawili wameambukizwa kama anavyotanabahi George Njogopa:

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)