Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 2,000 wakimbia ghasia nchini Ivory Coast

Watu 2,000 wakimbia ghasia nchini Ivory Coast

Karibu watu 2000 kutoka nchini Ivory Coast wamekimbilia Liberia na Guinea wakati mzozo wa ni nani aliibuka mshindi kwenye uchaguzi mkuu nchi humo ukiendelea kuchacha.

Shirika la kuwahuduumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linafuatilia kwa karibu hali kwenye taifa hilo la Afrika Magharibi ambapo Rais wa zamani Laurent Gbagbo amekataa kukubali kushindwa na kiongozi wa upinzani Alassane Outtara. Msemaji wa UNHCR Andrej Mahecic anasema kuwa mashirika yanawatembelea wakimbizi waliopewa makao kwenye vijiji maskini vilivyo kwenye mipaka

(SAUTI YA ANDREJ MAHECIC)