Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauaji ya halaiki yaendelea Darfur:ICC

Mauaji ya halaiki yaendelea Darfur:ICC

Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC amesema kuwa mauaji ya halaiki bado yanaendelea katika jimbo la Darfur nchini Sudan na kuwa Rais wa nchi hiyo Omar al-Bashir ambaye amepewa waranti wa kukamatwa na mahakama hiyo anaendelea kuficha na kuihadaa jamii ya kimataifa.

Luis Moreno Ocampo ameliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwa serikali ya Sudan haishirikiani na mahakama ya ICC au kuwachukulia hatua zozote wahusika wa vitendo vya mauaji ya halaiki. Ocampo amesema kuwa kwa miezi sita iliyopita mamia ya raia katika jimbo la Darfur waliuawa na maelfu ya wengine kulazimishwa kuhama makwao huku zaidi ya watu milioni mbili wakiendelea kuteseka. Mwezi Julai mwaka huu mahakama ya ICC ilitangaza waranti wa pili wa kukamatwa kwa Rais Bashir kutokana na mashtaka ya uhalifu wa kivita katika jimbo la Darfur.