Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vitisho kwa taarifa za mitandaoni havifai- Navi Pillay

Vitisho kwa taarifa za mitandaoni havifai- Navi Pillay

Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadamu siyo jambo la haki kuendelea kuandamana mtandao mmoja ambao umechapisha ripoti za siri zinazohusu utendaji wa serikali ya Marekani.

Navi Pillay amesema kuwa utumiaji wa lugha za vitisho, kuwepo kwa nguvu kubwa siyo ishara njema hasa kwa kuzingatia kuwa sheria mbalimbali za kimataifa zipo na zinaweza kutumika kama mhusika wake atabainika ametenda makosa.

 

Tangu kutolewa kwa taarifa mbalimbali zinazohusu utendaji wa serikali ya Marekani mmiliki wa mtandao huo wa WikiLeaks amekuwa akiandamwa vikali ikiwemo Marekani yenyewe.

 

Navi Pillay anataka suala hilo lishughulikiwe kwa kufuata mifumo ya sheria na siyo utoaji vitisho vinavyozidi mpaka upande wa tatu