Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aweka msukumo kwenye kampeni ya usafiri salama

Ban aweka msukumo kwenye kampeni ya usafiri salama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameipa nguvu kampeni ya kuwa na usafiri salama barabarani na kuhimiza namna inavyowezekana kuwa na usafiri imara na salama.

Ban amekutana na balozi wa Oman kwenye Umoja wa Mataifa ambaye nchi yake imekuwa ikifadhilia maazimio mbalimbali ya Umoja huo yanayohusika na usalama bara barani.

 

Amesema kukosekana umakini barabarani ni changamoto kubwa inayoikabili dunia hivi sasa kwani kila siku karibu watu 3,500 hupoteza maisha na wengine wakisababishiwa vilema vya maisha.

 

Hivyo ametaka kila mamlaka kufanya juhudi kuondosha tatizo hilo ikiwemo pia kushiriki kwenye kampeni za kuhamasisha usafiri salama.