Waburundi sasa watangaza kuachana na siasa za uhasama

10 Disemba 2010

Wananchi wa Burundi wametangaza kuwa sasa wanaachana na matukio ya kihasama na vurumani ambayo hapo awali yalitumika kama ngao ya kuweza kufikia shabaya ya kisiasa.

Kulingana na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Charles Petrie amesema kuwa wananchi hao sasa wameanza kukaribisha utashi mpya wa maridhiano na maelewano.

 

Akizungumza kwenye kikao cha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, Bwana Petrie amesema kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto za hapa na pale zinazoibuliwa na makudi kadhaa ya upinzani lakini hata hivyo kuna ishara njema ya kuimarika kwa hali ya kisiasa.

 

Amesema kwa kufuatilia zoezi la uchaguzi uliopita, kuna toa matumaini kwamba sasa kuna uhuru wa kweli na hata nafasi ya vyama vya kirai   kwenye ujenzi wanchi hiyo sasa imeanza kuonekana.

 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter