Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka Liu Xiabao kuachiliwa huru

UM wataka Liu Xiabao kuachiliwa huru

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ameitaka serikali ya China kumuachiliwa huru mshindi wa tuzo la amani anayezuiliwa Liu Xiaobo.

Navi Pillay anasema kuwa alikuwa na matumani kuwa serikali ya china ingekuja kutambua umuhimu walio nao watu kama Liu Xiabo katika maendeleo ya Uchina. Akiongea mjini Geneva kabla ya siku ya kimataifa ya haki za binadamu Pillay ameelezea hisia zake kuhusiana na kukamatwa na kuzuiliwea kwa bwana Xiabo na washirika wa karibu kufutia kuteuliwa kwake kama mshindi wa tuzo la amani la mwaka 2010. Ameongeza kuwa katika majuma machache yaliyopita ripoti zimefichua kuwa takriban wanaharakati 20 wamekamatwa na kuzuiliwa na wengine zaidi ya 120 kuwekwa kwenye vizuizi vya nyumbani.