Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufisadi watishia maendeleo, utulivu na demokrasia :Ban

Ufisadi watishia maendeleo, utulivu na demokrasia :Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa ufisadi ni kitishio kikubwa kwa maendeleo na demokrasia. Akiongea wakati wa maadhimisho ya siku ya kupambana na ufisadi Ban amesema kuwa Umoja wa Mataifa unafanya kila uwezalo kuhakikisha kuwa ufisadi umeangamizwa kote duniani.