Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka kukomeshwa kwa vurugu nchini Haiti

Ban ataka kukomeshwa kwa vurugu nchini Haiti

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametaka kukomeshwa mara moja kwa vitendo vya vurugu nchini Haiti ambavyo vimezuka kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya awali ya ubunge.

Vurugu hizo zinaiweka nchi hiyo kwenye majaribu makubwa kwani mapema mwaka huu ilikubwa na matukio ya kusikitisha yakiwemo tetemeko kubwa la ardhi na baadaye kukazuka ugonjwa wa kipindupindu uliopoteza mamia ya maisha ya watu.

Akizungumzia vurumai hizo, Ban ametaka kuwepo kwa hali ya amani hasa katika kipindi hiki ambacho nchi hiyo inasaka majibu ya kutanzua matatizo yaliyoletwa na tetemeko la ardhi pamoja na nanma ya kuudhibiti ugonjwa wa kipindupindu.

Amesema amevunjwa moyo kutokana na kuendelea kuwepo kwa matukio hayo ya ghasia ambayo amesema yanakwamisha juhudi za kuitaka kuijenga upya nchi hiyo kwenye maeneo ya demokrasia na maendeleo.