Wawekezaji binasfi watakiwa waongeze fedha za kuimarisha uhifadhi wa mazingira

8 Disemba 2010

Mtafiti mmoja kutoka nchi za Ulaya amependekeza kuwa ni vyema wawekezaji binafsi waongezee ufadhili wao wa fedha ili kufanikisha miradi ya uhifadhi wa mazingira na ameongeza kuwa ufadhili huo unatakika ufikie hadi asilimia 90.

 Wajumbe mbalimbali duniani kote wanaendelea na majadiliano kwenye mkutano huko Cancun, Mexico wakiwa na matumaini ya kufikia makubaliano yenye tija ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

 

Mtafiti Ole Beier Sorensen kutoka taasisi ya wawekezaji binasfi wanaojishughulisha na mazingira amesema kuwa ili kuwashirikisha kikamilifu kwenye miradi ya kukwamua mazingira, lazima kwanza wawekezaji hao wawe na ufahamu wa kutosha kuhusu suala hili la mabadiliko ya hali ya hewa na uhifadhi wa mazingira.

.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter