Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Changamoto za kuwalinda waliohama makwao na wakosa uraia kuongezeka:Guterres

Changamoto za kuwalinda waliohama makwao na wakosa uraia kuongezeka:Guterres

Mkuu wa tume ya wakimbizi ya Umoja wa Mataifa António Guterres ameonya kuwa kunaendelea kushuhudiwa changamoto katika kuwalinda mamilioni ya watu waliolazimishwa kuhama makwao pamoja na wakosa uraia na kuitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za dharura.

Akihutubia mkutano wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa mjini Geneva Guterres amesema kuwa kuongezeka kwa watu, mabadiliko ya hali ya hewa, uhaba wa maji na chakula vimesababisha kuwepo kwa mizozo na kufanya watu kukimbia nchi zao. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)