Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atoa wito kwa makubaliano mapya ya kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa

Ban atoa wito kwa makubaliano mapya ya kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito wa kuafikiwa kwa makubaliano kwenye mkutano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa unaondelea mjini Cancun Mexico na kuwataka wajumbe kwenye mkutano huo kujua kuwa kucheleweshwa kwa makubaliano kunaiweka hatarini afya ya dunia, uchumi wa dunia na pia kwa wanadamu.

Ban amesema kuwa ameshangazwa kutokana na kuwa hakujakuwa na jitihada hata baada ya miaka mingi ya majadiliano bado suluhu kamili halijapatikana. Nchi nyingi zilizostawi zilikubaliana kupunguza gesi zinazochafua mazingira zinazosababisha kuwepo kwa mabadiliko ya hali ya hewa kama moja ya makubaliano ya Kyoto yanayofikia mwisho mwaka 2012. Ban sasa anataka kujadiliwa kwa maafikiano mapya.

(SAUTI YA BWANA BAN KI-MOON)