Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afisa wa UM ataka haki zaidi kwa wanawake

Afisa wa UM ataka haki zaidi kwa wanawake

Kuanzishwa kwa kitengo maalumu ndani ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wanawake, kumeelezwa kuwa ni ukombozi tosha utakaoweza kuwakwamua wanawake hao.

Anne Marie Goetz ambaye ni mshauri mkuu katika chombo kijulikanacho UNIFEM amesema kuwa kwa miaka mingi masuala yanayohusu wanawake yamekuwa hayapewi umuhimu wowote licha kwamba mchango wao kwenye jamii ni wa kiwango cha hali ya juu.

Ameeleza kuwa kuanzishwa kwa kitengo kinachohusika na masuala ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji kwa wanawake ndani ya Umoja wa Mataifa kutasaidia kujibu kero na shuruba zinazoendelea kuwakabili wanawake duniani kote.

Aidha ametaka jumuiya mbalimbali za kimataifa kutokuyapa kisogo masula yanayohusu wanawake akisema kuwa wanawake ni tunu yenye mchango mkubwa hivyo lazima itambuliwe na kutendewa haki.