Chanjo mpya dhidi ya ugonjwa wa pneumonia kuzinduliwa

Chanjo mpya dhidi ya ugonjwa wa pneumonia kuzinduliwa

Chanjo mpya ya kuzuia aina kadha hatari za ugonjwa wa Pneumonia ambao ndio ugonjwa unaosababisha vifo vingi zaidi miongoni mwa watoto kote duniani itazinduliwa nchini Nicaragua wiki ijayo.

Dawa hii itatumika kuwachanja watoto kwenye nchi tajiri na pia maskini. Dawa hii yenye thamani ya dola 90 nchini Marekani na dola 53 barani ulaya pia itapatikana kwenye nchi zinazoendelea kwa bei ya chini kidogo.

Inatarajiwa kuwa dawa hiyo itazuia vifo 700,000 kati ya sasa na mwaka 2013. Nchi 13 zikiwemo Kenya , Sierra Leone na jamhuri ya kidemokrasi ya Congo pamoja na mali zitapokea dawa hiyo