Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO kutoa mpangilio wa viwango vya madawa ya kienyeji

WHO kutoa mpangilio wa viwango vya madawa ya kienyeji

Shirika la afya duniani WHO linatarajiwa kuanzisha mpango wa kwanza kabisa ya kuyatambua madawa ya kienyeji na kutambua manufaa yake.

Naibu mkurugenzi wa masuala ya habari na utafiti katika shirika la WHO Marie-Paule Kieny anasema kuwa wanakubali kuwa madawa ya kienyeji yanatumika kwa wingi hususan kusini mashariki mwa Asia , Afrika na Amerika kusini. Utafiti wa WHO kote duniani hasa Ulaya na Marekani unaonyesha kuwa matumizi ya madawa ya kienyeji yanaendelea kuongezeka. Christie Fieg ni kutoka WHO:

(SAUITI YA CHRISTIE FIEG)"