Skip to main content

Kipindi cha miezi miwili ijayo itakuwa wakati muhimu kisiasi Myanmar: Ban

Kipindi cha miezi miwili ijayo itakuwa wakati muhimu kisiasi Myanmar: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa hali ya kisiasa nchini Myanmar katika kipindi cha miezi miwili ijayo inakabiliwa na wakati mgumu.

Bwana Ban ambaye alikuwa akizungumza kwenye hafla moja iliyowajumuisha kundi la watu linalojulikana kama marafiki wa Myanmar amesema ni lazima sasa mamlaka husika kuanza kuyashirikisha makundi hayo yaliyotengwa kwenye uchaguzi huo.

Amesema wasiwasi wan chi hiyo kukosa uungwaji mkono toka jumuiya za kimataifa ni mkubwa kama itaendelea kuyapuuza makundi hayo ya kisasa.