Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yahofia hali kuwa mbaya zaidi nchini Pakistan wakati wa msimu wa baridi

UNICEF yahofia hali kuwa mbaya zaidi nchini Pakistan wakati wa msimu wa baridi

Hali mbaya ya kimazingira bado inawaandama wananchi wa Pakistani ikiwa ni miezi nne sasa tangu nchi hiyo ishuhudie mafuriko makubwa ya mvua yaliyoleta maafa makubwa.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalishughulika na watoto UNICEF limeonya kwamba huenda hali ikawa mbaya zaidi kwa watoto hasa kwenye kipindi cha majira ya baridi.

Takwimu zinaonyesha kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la matatizo ya kiafya kwa watoto wengi ikiwemo kuzuka kwa ugonjwa wa polio.

Hata hivyo jumuiya za kimataifa zimeanza kuchukua jukumu la haraka kama kuanza kusambaza nguo, mablanketi na vifaa vingine vya kujikumu wakati huu wa kuelekea msimu wa baridi.