Skip to main content

Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu inahitaji kuungwa mkono: BAN

Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu inahitaji kuungwa mkono: BAN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amezitaka nchi zote kuiunga mkono mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC ili kuweza kupigana na kutochukuliwa hatua za kisheria dhidi ya watu wanaohusika na uhalifu.

Akiongea mjini New York Ban amesema kuwa mahakama hiyo inakumbwa na changamoto nyingi. Amesema kuwa bado mahakama hiyo haipati uungwaji mkono na kuna utata wa jinsi inavyoweza kuendesha shughuli zake. Amesema kuwa ikiwa ulimwengu uko tayari kumaliza mazoea ya kukwepa mkono wa sheria na kuleta uwajibikaji ni lazima mahakama hiyo iungwe mkono.