Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wapakistani wahitaji usaidizi zaidi:UM

Wapakistani wahitaji usaidizi zaidi:UM

Afisa wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kibinadamu amewatembelea waliothirika na mizozo kaskazini magharibi mwa Pakistan na kutoa wito kwa misaada zaidi ya kibinadamu kwa watu hao ambao wengi kati yao wameelezea nia ya kurejea makwao.

Akiwa kwenye siku ya nne na ya mwisho ya ziara yake nchini Pakistan Valeria Amos amesema kuwa wengie wa aliokutana nao walikuwa na nia ya kurudi makwao ili kuendelea na shughuli zao. Amos amesema kuwa baadhi ya watu walioathirika walikuwa wakimbizi na ambao kwa sasa wamekumbwa na janga la mafuriko.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI.)

Bi Amos aliitembelea kambi ya Jalozai ambapo karibu wanaume na wanawake na watoto 97,000 wanaishi kwenye mahema na kupata maji safi ya kunywa , chakula , elimu na huduma zingine. Wengi wa wakaazi wa kambi hiyo walitoroka makwao kutokana na mzozo uliokuwa eneo la kaskazini lenye makabila huku wengine wakiwasili katika kambi hiyo zaidi ya miaka miwili iliyopita. Mafuriko yaliyoikumba Pakistan mwezi Julai yamesababisha majanga makubwa kuwahi kuhudumiwa na Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kutoa huduma za kibinadamu. Mashirika ya kutoa misaada yamekusanya misadaa itakayopelekewa mamilioni ya watu kwenye maeneo yaliothirika. Hata hivyo misaada zaidi inahitajika kuwasaidia watu kurejea kwenye shughuli zao za kilimo na kujenga makao.