Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Masuala ya ukatili dhidi ya wanawake yatatuliwa kupitia malengo ya maendeleo ya milenia: UM

Masuala ya ukatili dhidi ya wanawake yatatuliwa kupitia malengo ya maendeleo ya milenia: UM

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya ukatili dhidi ya wanawake Rashida Manjoo amesema kuwa ukatili dhidi ya wanawake kote duniani umekita mizizi.

Ukatili dhidi ya wanawake pia umetajwa na wengi kuwa lengo la maendeleo ya milenia lililokosa miongoni mwa malengo hayo huku harakati za kukabiliana na suala hilo zikikumbwa na changamoto zikiwemo za hali mbaya ya uchumi duniani au kutumika kwa ukatili dhidi ya wanawake kama silaha wakati wa mizozo. Kwa muda wa miaka kumi iliyopita hatua zimepigwa katika baadhi ya malengo ya millennia lakini hata hiyo ukosefu wa usawa na kuwatenga wanawake na wasichana limesalia kuwa changamoto kubwa.