Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mataifa maskini yanaweza kuziba pengo la ukosefu wa chakula

Mataifa maskini yanaweza kuziba pengo la ukosefu wa chakula

Shirika la kimataifa la kilimo na mandeleo IFAD linasema kuwa watu wanaoishi katika hali ya umaskinmi vijijini kwenye nchi zinazoendelea huenda wakanufaika na mahitaji ya chakula duniani Kulingana na ripoti ya IFAD ni kuwa wakulima kwenye nchi maskini duniani watatoa mchango mkubwa wa kuzalisha chakula kwa watu wa mijini.

(SAUTI YA ED HEINEMANN)

"Tunahitaji kufanya kazi na wakulima wadogo kuwasaidia kufikia masoko hususan masoko ya mijini.Tunahitaji kuwasaidia kutumia mbinu za kilimo ambazo kwa njia moja zina mazao zaidi na pia zina gharama ndogo"