Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanajeshi wa zamani ahukumiwa kifungo cha maisha Rwanda

Mwanajeshi wa zamani ahukumiwa kifungo cha maisha Rwanda

Aliyekuwa wakati mmoja mwanajeshi wa ngazi ya juu nchini Rwanda amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani na mahakama ya kimataifa inayowahukumu waliohusika na mauaji ya halaiki nchini Rwanda mwaka 1994.

Ildephonse Hategekimana, aliyekuwa luteni katika jeshi la Rwanda alipataka na makosa matatu ya kuwauwa watu wa kabila la watusi alipokuwa kamanda. Hategekimana pia alipatikana na hatia ya ukiukaji wa haki za binadamu na kuwaua watusi na pia ubakaji. Alikamatwa mwezi Februari mwaka 2003 nchini Congo Brazzaville na kupelekwa katika makao makuu ya mahakama hiyo mjini Arusha nchini Tanzania.