Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aelezea hisia zake kuhusu kuzorota kwa hali nchini Ivory Coast.

Ban aelezea hisia zake kuhusu kuzorota kwa hali nchini Ivory Coast.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amelezea hisia zake kuhusiana na hali ilivyo nchini Ivory Coast hata baada ya kundeshwa kwa uchaguzi uliokuwa wazi na matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi kuungwa mkono na ujumbe wa Umoja wa Mataifa.

Kupitia kwa msemaji wake Ban anasema kuwa matokeoa ya uchaguzi huo wa urais yalithibitishwa kuwa huru na mjumbe wake maalum na pia yamekubaliwa na jamii ya kiamataifa. Ban amekariri wito wake kwa wananchi wa Ivory Coast kuwa watulivu na wavumilivu na kuongeza kuwa Umoja wa Mataifa utafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwepo kwa usalama na amani nchini Ivory Coast. Mkuu wa Redio ya Umoja wa Mataifa Sylvain Semilinko anasema kuwa hali imesalia kuwa tete.

(SAUTI YA SYLVAIN SEMILINKO)