Chanjo mpya yatarajiwa kutokomeza ugonjwa hatari wa homa ya uti barani Afrika

Chanjo mpya yatarajiwa kutokomeza ugonjwa hatari wa homa ya uti barani Afrika

Burkina Faso limekuwa taifa ya kwanza kuanzisha kampeni ya chanjo mpya ya nchi nzima dhidi ya homa ya uti wa mgongo iliyo na lengo la kuangamiza chanzo cha ugonjwa huo.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Eneo la kusini mwa jangwa la sahara ndilo lilipigwa zaidi na ugonjwa huo na inakadiriwa kwamba zaidi watu milioni 450 wapo hatarini kwa sasa.

Burkina Faso ikiwa moja ya nchi za afrika ambazo zinashambuliwa mara kwa mara, imepongeza hatua iliyobuniwa wenye shabaya ya kuufanya ugonjwa huo unatoweka kabisa.

Kwa mujibu wa Waziri wa afya Seydou Bouda makubaliano ya pamoja yaliyofikiwa na mawaziri wa afya barani afrika ni hatua ya kwanza inayotoa picha ya ushindi dhidi ya ugonjwa huo.

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali limeanzisha mpango maalumu wa utoaji chanjo ambayo inakusudia kusambazwa katika maeneo mbalimbali ya afrika.

Wengi wanaokumbwa na ugonjwa wa uti wa mgongo wanapoteza maisha lakini hata wale wananusurika wanakabiliwa na matatizo kadhaa ya kiafya ikiwemo kuharibika kwa milango ya fahamu kwenye ubongo