Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Njia ya kuafikia makubaliano ya Cancun yaanza kujitokeza-UM

Njia ya kuafikia makubaliano ya Cancun yaanza kujitokeza-UM

Vyombo vya Umoja wa Mataifa vinavyoshughulikia mpango wa uratibuji mazingira vinamatumaini kwamba mkutano wa Cancún, Mexico ambao unajadilia changamoto za mazingira huenda ukifikia makubaliano ya kupitisha azimio jipya hapo Ijumaa.

Miongoni mwa mambo yaliyofikiwa ni kuendelea kutoa uungwaji mkono wa hali na mali kwa nchi zinazoendelea ili ziweze kutekeleza miradi ya kuhifadhi mazingira.

Wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa wanamatumaini kuwa mkutano huo wa Cancun utapata mafanikio makubwa na kufikia mabonde yaliyoashwa wakati wa mkutano uliopita wa Copenhagen.