Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban awapongeza wafanyakazi wa kujitolewa duniani kote.

Ban awapongeza wafanyakazi wa kujitolewa duniani kote.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametiwa moyo na makundi ya watu wanaofanya kazi za kujitolea kwa ajili ya kuhamasisha masuala ya amani na utulivu duniani kote.

Ban amewapongeza wafanyakazi hao wanaofikia zaidi ya milioni moja akisema kuwa mchango wao unadhamani kubwa mbele ya uso wa dunia kwani wanaendelea kujitolea ili kusukuma mbele masuala ya uletaji maendeleo na kuhimiza amani na utengamao

Ametaka jumuiya za kimataifa kuanzisha taasisi ambazo zitafanya kazi kwa pamoja na makundi hayo ya kujitolea kwa lengo la kuviongezea uwezo wa ufanyaji kazi.

Hata hivyo ameeleza kuwa jukumu la kufanya kazi za kujitolewa halina mipaka kwani milango imefunguliwa kwa kila atakaye. Amezungumzia pia kupanuka kwa wigo wa kazi za kujitolewa kupitia mifumo ya mitandao ya mawasiliano.