Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bila kuwakwamua walemavu hatuwezi kutokomeza umasikini:Ban

Bila kuwakwamua walemavu hatuwezi kutokomeza umasikini:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezitolea wito serikali zote kuongeza juhudi kuwasaidia walemavu kwani amesema bila kutatua matatizo yao , vita dhidi ya umasikini, maradhi na maendeleo duni hatuwezi kuvishinda.

Na ulemavu sio kulemaa bali wanasema wanahitaji msaada wa hali na mali kuwawezesha kutikimu kimaisha na kujitegemea.

Flora Nducha katika makala y leo anaangalia maisha ya walemavu afrika ya Mashariki, changamoto gani zinawakabili, kwa nini kila siku wanajikuta wakisalia katika hali ya umasikini na je wanaona nini kifanyike kuwakwamua katika hali hiyo? Ungana naye.