Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi waliorejea Iraq wanakabiliwa na matatizo:IOM

Wakimbizi waliorejea Iraq wanakabiliwa na matatizo:IOM

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limesema kuwa, hali ya maisha kwa kinamama ambao walirejea nyumbani kuanza maisha mpaya ni mbaya kupindukia wakikabiliwa na shida kama ukosefu wa chakula afya duni na kukosa kazi.

Taarifa ya shirika hilo imesema kuwa wanawake wengi ambao walikuwa mtawanyikoni na baadaye kuamua kurejea nyumbani wanakabiliwa na changamoto kubwa kwani licha ya kuwa na jukumu la kusimamia familia zao lakini wanajikuta kwenye hali mbaya zaidi kutokana na kukosa huduma bora za kijamii

Pamoja na kwamba mamlaka nchini humo zimetoa kadi ya vitambulisho zinavyotumika kwa ajili ya kupatiwa huduma, lakini hata hivyo ni wachache sana wanaoweza kufaidika na mpango huo.

Wengi wao wanakabiliwa na ukosefu wa huduma za kiafya, chakula na kukosa maeneo ya kufanyia kazi jambo ambalo limetatiza mambo mengine mbalimbali.