Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upungufu wa fedha kukabili hali ya hewa una athari:FAO

Upungufu wa fedha kukabili hali ya hewa una athari:FAO

Mafuriko na ukame katika nchi ambazo ni wazalishaji wakubwa wa chakula kwa mwaka huu yamesababisha kupanda kwa bei za chakula, ikiashiria hatari iliyopo katika mfumo wa uzalishaji wa chakula duniani na masoko ya kilimo.

Hali hiyo inaweza ikatokea mara kwa mara na kusababisha athari kubwa katika miaka ijayo kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Ingawa kuna mifano mingi ya jinsi kilimo kinavyoweza kuhimili matatizo ya hali ya hewa ufadhili unasalia kuwa tatizo kubwa. Jayson Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JAYSON NYAKUNDI)

Mkurugenzi katika idara ya mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa kwenye shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO Peter Holmgren anasema kuwa ufadhili uliopo kwa sasa hautoshi kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa zinazokabili sekta ya kilimo.

Fedha zinazotengewa sekta ya kilimo kwenye nchi zinazoendelea ni kidogo hata kama kilimo huwa kinachangia asilimia 29 ya bato lote la kitaifa. Fedha zitakazotumika kila mwaka katika kilimo kwenye zionazoendelea ili kufuatana na mabadiliko ya hali ya hewa zinakadiriwa na benki ya dunia kuwa zitakuwa kati ya dola bilioni 2.5 na dola bilioni 2.6 kati ya mwaka 2010 na 2050.

Hii ndiyo moja ya ajenda kuu FAO inawasilisha kwenye mkutano wa kila mwaka wa mabadiliko ya hali ya hewa unaoendelea mjini Cancun nchini Mexico.