Valarie Amos arejea Pakistan kuwahakikishia msaada:OCHA

Valarie Amos arejea Pakistan kuwahakikishia msaada:OCHA

Miezi minne baada ya mafuriko mabaya kuwahi kuikumba Pakistan msaada wa kibinadamu bado unahitajika.

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala kibinadamu OCHA Valerie Amos yuko nchini humo kwa mara ya pili kwa ziara ya siku tatu. OCHA inasema lengo la ziara yake ni kusisitiza jukumu la Umoja wa Mataifa la kuendelea kuwasaidia watu wa Pakistan ambao walikumbwa na mafuriko ya kihistoria miezi minne iliyopita.

Akiwa nchini humo Bi Amos atazuru majimbo ya Sind na Khyber Pakhtunkwa ambayo yaliathirika vibaya zaidi na mafuriko hayo. Pia atakutana na maafisa wa serikali, wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali na wa Umoja wa Mataifa.