Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi wa dunia hautoimarika kwa mwaka ujao:UM

Uchumi wa dunia hautoimarika kwa mwaka ujao:UM

Uchumi wa dunia unatarajiwa kukua kwa kiwango kidogo mwaka ujao wakati uanakadiriwa kuimarika kwa asilimia 3.1 mwaka 2011 na kwa asilimia 3.5 mwaka 2012.

Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa ni kuwa viwango hivyo havitaweza kuchangia kapatikana kwa nafasi za ajira zilizopotezwa wakati hali mbaya ya uchumi ilipoikumba dunia. Ripoti hiyo inasema kuwa kati ya mwaka 2007 na 2009 takriban watu milioni 30 walipoteza ajira kote duniani kufuatia hali mbaya ya uchumi iliyoikumba dunia.

Mkurugenzi wa idara ya masuala ya uchumi na jamii ya Umoja wa Mataifa DESA, Rob Vos ambaye aliongoza kundi la wana uchumi wa Umoja wa Mataifa kuandaa ripoti hiyo anasema kuwa bado kuna hali ngumu katika siku za usoni. Vos anasema kuwa ukuaji ya uchumi ulioshuhudiwa kati kati ya mwaka 2009 ulianza kuzoroka mwaka huu kutokana na unyonge wa nchi zilizostawi.