Skip to main content

Waathirika wa ukimwi Eldoret Kenya wanufaika na msaada wa bure wa kisheria

Waathirika wa ukimwi Eldoret Kenya wanufaika na msaada wa bure wa kisheria

Wakati dunia ikiwa imeadhimisha siku ya ukimwi duniani hapo jana kwa akuali mbiu ya fursa na haki za binadamu, msaada wa kisheria kwa waathirika wa ukimwi wakati mwingine inaweza kuwa changamoto kubwa, lakini sasa nchi mbalimbali zimeanzisha mipango ya kuwasaidia waathirika wasiojiweza kulipia gharama.

Nchini Kenya kituo cha usaidizi wa kisheria legal aid center of eldoret(LEC) kilichoko magharibi mwa nchi kinawasaidia maelfu ya waathirika wa ukimwi wanaohitaji msaada wa kisheria bure bila gharama yoyote katika masuala mbalimbali ikiwemo ya talaka, ukatili dhidi ya wanawake, kubakwa, haki ya kumiliki nyumba na mali na hata kumiliki watoto.

Avril Rua ni miongoni mwa mawakili katika kituo hicho ambaye amezungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii na kumfafanulia wanachofanya.