Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko ya jana Darfur yanastahili kuchunguzwa Ban.

Machafuko ya jana Darfur yanastahili kuchunguzwa Ban.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-Moon ametoa wito wa kufanyika uchunguzi wa tukio la jana ambalo limesababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi wengine baada ya waandamanaji kupambana na jeshi la ulinzi na usalama la Sudan kwenye chuo kikuu jimbo la Darfur.

Tukio hilo lilitokea wakati mpatanishi mkuu wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika Djibril Bassole na waziri wa mambo ya nje wa Qatar Ahmed bin Abdulla Al-Mahmoud wakikutana na wawakilishi wa jumuiya za kijamii kwenye chuo kikuu cha Zalingei.

Ban amesema amesikitishwa na kupotea kwa uhai na ametoa wito wa kufanyika uchunguzi kupata ukweli wa tukio hilo, ameongeza kuwa pande zote katika mgogoro wa Darfur na watu wote wa jimbo hilo wana haki ya kutoa mawazo yao kwa uhuru na uwazi.