Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umezindua ombi la msaada kwa ajili ya Wapalestina.

UM umezindua ombi la msaada kwa ajili ya Wapalestina.

Maisha ya kila siku kwa Wapalestina wanaoishi Gaza bado ni magumu licha ya Israel kulegeza vikwazo kwenye ukanda wa Gaza ambavyo vimeruhusu bidhaa zaidi kuingia katika ukanda huo kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Zaidi ya asilimia 75 ya Wapalestina wanaoishi Gaza wanategemea misaada ambayo ni pamoja na chakula,,alazi na fedha. Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya eneo linalokaliwa na Wapalestina. Maxwell Gaylard amesema mashirika yanahitaji takribani dola milioni 575 katika kipindi cha mwaka mmoja ujao ili yaweze kutoa msaada unaohitajika kwa Wapalestina.

(SAUTI YA MAXWELL GAYLARD)

Bwana Gaylard amesema wakipewa fursa Wapalestina wanauweze wa kujenga mfumo mzuri wa kusafirisha bidhaa nje ambao utasaidia kuinua uchumi, kupunguza umasikini na tatizo la ajira.