Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utumwa bado unafumbiwa macho majumbani duniani:UM

Utumwa bado unafumbiwa macho majumbani duniani:UM

Leo ni siku ya kimataifa ya kukomesha utumwa, ambayo ilitengwa maalumu na mkataba uliopitishwa na baraza kuu la Umoja wa Mataifa tarehe pili December mwaka 1949.

Akitoa ujumbe maalumu kuhusu kuadhimishwa kwa siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema mfumo wa kisasa wa utumwa ni kosa la jinai na ameitaka jumuiya ya kimataifa kuwa makini na kuongeza juhudi kutokomeza kabisa mfumo wa kisasa wa utumwa.

Ban ameongeza kuwa waathirika na manusura wa utumwa wanahaki ya kulindwa na kuthaminiwa utu wao. Naye mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mifumo ya kisasa ya utumwa Bi Gulnara Shahinian amesema wafanyakazi wa majumbani ambao wananyanyasika iwe kimwili, kihisia au hata kimapenzi wanatendewa kama watumwa.

Amesema mfumo huu wa utumwa unafanyika duniani kote ingawa waathirika kwa kiasi kikubwa hawaonekani mbele ya macho ya jamii jambo ambalo amesema linatia hofu hasa katika haki za binadamu. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)