Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msumbiji yapewa heko katika mipango ya kilimo:WFP

Msumbiji yapewa heko katika mipango ya kilimo:WFP

Msumbiji imetajwa kwamba ni nchi ya kupigiwa mfano iliyoweza kufanya mageuzi ya haraka na ya kiubunifu kwenye eneo la kukabiliana na tatizo la njaa.

Akitoa pongezi zake kwa serikali ya Msumbiji, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la chakula la Umoja wa Mataifa WFP, Josette Sheeran amesema mpango unaendeleshwa na serikali unaojulikana kama nunua kwa maendeleo, ambao unawaunganisha wakulima wadogo kwenye masoko mazuri, umesaidia nchi hiyo kuwa na uzalushaji bora wa chakula na kuwa na hifadhi ya kutosha.

Mpango huo ambao ulibuniwa na Shirika hilo la Umoja wa mataifa WFP kwa njia ya kuongeza uzalishaji wa chakula na chenye ubora wa hali ya juu, umeweza kusaidia nchi hiyo kuondokana na tatizo la ukosefu wa chakula na wakulima wake wameendelea kuutekeleza kwa ufanisi mkubwa.

Kupitia mpango huo,WFP imeweza kubadilisha mkondo wa mambo kwa kununua chakula kingi barani afrika na hatimaye kukitawanya kwenye maeneo yenye uhitaji tofauti na miaka ya nyuma ambapo chakula kingi kikipatikana toka nchi zilizoendelea.