Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia tofauti ya nishati kupunguza gesi chafu:UNEP

Teknolojia tofauti ya nishati kupunguza gesi chafu:UNEP

Kwa kuondoa mifumo ya kupata mwangaza isiyostahili mataifa yana uwezo wa kupunguza matumizi yao ya kawi, gesi zinazochafua mazingira na piz kupunguza gharama za kupata mwangaza kwa kutumia taa.

Kulingana na utafiti mpya wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP utakaowasilishwa hii leo kwenye mkutano wa hali ya hewa mjini Cancun Mexico uaneleza jinsi hewa chafu inaweza kupunguzwa kwa kutumia teknolojia tofauti kwenye nchi mia moja.

Inakadiriwa kuwa huenda nchi zaidi zikavutiwa na mabadiliko kwenye teknolojia ya kupata mwangaza na kuachana na njia zinazochangia kuwepo kwa gesi inayochafua mazingira. Kulingana na shirika la kimataifa la kawi umeme unaotumiwa kutoa mwangaza unachangia asilimia nane ya gesi inayochafua mazingira duniani.